HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 1, 2011

Kina Mama Wasusia Tendo la Ndoa hadi Barabara Iwekwe Sawa

Zaidi ya wanawake 250 wa mji mmoja nchini Kolombia wameanza mgomo wa kuwapa unyumba waume zao ili kuishinikiza serikali iifanyie marekebisho barabara inayoingia mjini humo.

Wanawake katika mji wa Barbacoas wanaamini kwamba iwapo wataanza mgomo wa "kuibana miguu yao" kwa kuwanyima unyumba waume zao, basi waume zao watalazimika kufanya jitihada za kuishinikiza serikali yao kuijenga barabara inayoingia mjini humo ambayo iko kwenye hali mbaya sana kiasi cha kuhatarisha maisha yao.

Kwa miaka 20, serikali iliahidi kuifanyia marekebisho ya barabara hiyo inaoingia kwenye mji wa Barbacoas ambao una jumla ya wakazi 40,000 lakini haijawahi kutimiza ahadi yake, limeripoti jarida la Wall Street Journal.

Hivi sasa inawachukua watu masaa 10 kuweza kusafiri umbali wa kilomita 56.

"Wanawake hawa na watu wote katika mji huu, tumechoshwa na ahadi hewa za serikali", alisema Lucelly Del Carmen Viveros, mtetezi wa haki za binadamu kwenye mji wa Barbacoas.

"Hii ndio barabara pekee inayouunganisha mji wa Barbacoas na miji ya karibu nchini lakini ipo katika hali mbaya sana", aliongeza Viveros.

kwa habari hizi na nyingine nyingi,bofya link hii.

2 comments:

  1. Kudadadekiizz huu mgomo ukija bongo hapa kwa kushinikiza Umeme,Barabara,Kupinga Ufisadi na Nk. itakuwa poa sana hasa kwa wale wajanja wachache.yaani nimeipenda sana hii.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad