HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 7, 2011

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI EXTRA LAGER 2011

Meneja Mauzo wa TBL,Fimbo Buttallah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangazwa kwa uzindizi wa mashindano ya ngoma za asili kwa mwaka 2011 yatakayofanyika katika mikoa mitano hapa nchini.kulia ni Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager,Edith Bebwa.
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager,Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo alipokuwa akizungumzia uzinduzi rasmi wa mashindano ya ngoma za asili yatakayofanyika katika mikoa mitano hapa nchini.kushoto ni Meneja Mauzo wa TBL,Fimbo Buttallah.

Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha BALIMI EXTRA LAGER imetangaza rasmi ufunguzi wa mashindano ya ngoma za asili kwa mwaka huu wa 2011.

Bia ya BALIMI EXTRA LAGER imekuwa mdhamini rasmi wa mashindano haya kwa zaidi ya miaka saba sasa. Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema meneja wa bia ya Balimi Extra Lager Bi Edith Bebwa.

Vile vile ni njia moja wapo kwa wakazi kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi zinazotolewa na bia ya Balimi Extra Lager.

Mashindano haya yatajumuisha mikoa mitano Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, Kagera na fainali kurudi tena jijini Mwanza.Maboresho makubwa yamefanyika katika mashindano haya ya mwaka 2011 ukilinganisha na yale ya mwaka jana. Zawadi zimeongezeka mara dufu. Hii ni kuwapa changamoto wakazi wa kanda ya ziwa kushiriki zaidi kwenye mashindano haya ya ngoma za asili za mwaka 2011.
Kwa niaba ya TBL kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra Lager tunawakaribisha wote kushuhudia michuano hii na vilevile waburudike na Balimi Extra lager. Zaidi tunavitakia heri vikundi vyote vitakavyoingia kwenye mashindano haya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad