HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 7, 2011

KIWANDA CHA MADAWA CHA KEKO CHAKABIDHI ZAWADI YA GARI KWA MSAMBAZAJI ALIYEVUKA LENGO LA MANUNUZI TANZANIA 2010

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampini ya utengenezaji madawa ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Mercy Marealle akimkabidhi gari aina ya Toyota Nadia,Riyaz Gangji ambae ni mshindi wa manunuzi ya Dawa zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwa mwaka 2010.

Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Flora Kessy akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna walivyoweza kuendesha droo ya kumpata mshindi wa manunuzi ya dawa leo katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya kampuni hiyo,Keko jijini Dar.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampini ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Mercy Marealle na kulia ni Meneja wa IT na Mauzo wa kampuni hiyo,Alfonce Macha.

Mshindi wa gari aina ya Toyota Nadia kutoka  na kampuni ya ABBAS EMPORIUM,Riyaz Gangji akizumza na vyombo vya habari juu ya ushindi alioupata leo.kulia ni Mwanae Riyaz akiwa ni mwenye furaha baada ya baba yake kushinda gari hilo.

Baadi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Kutengeneza Dawa ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi Gari aina ya Toyota Nadia kwa Mshindi wa manunuzi ya dawa zinazotengenezwa na kampuni hiyo iliyofanyika mapema leo asubuhi.

Baadhi ya Wanahabari na Wafanyakazi wa kampuni ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES wakiwa katika hafla hiyo leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampini ya utengenezaji madawa ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Mercy Marealle (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Manunuzi ya Dawa,Riyaz Gangji (tatu kulia) pamoja na ndugu zake na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi gari kwa mshindi huyo mapema leo asubuhi katika viwanja vya kampuni hiyo,Keko jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad