HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 3, 2011

FILAMU YA CHUMO YAZINDULIWA JIJINI DAR

Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Filamu ya CHUMO,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dr. Haji Mponda akitoa hotuba ya uzinduzi wa Filamu hiyo inayoelezea athari za ugonjwa wa Malaria,Uzinduzi huo umefanyika usiku huu katika hoteli ya Movenpick jijini Dar.
Mtengenezaji Kiongozi wa Filamu hiyo,Jordan Riber akizungumza na vyombo vya habari kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo katika hoteli ya Movenpick usiku huu.
Mkuu wa Mradi wa COMMIT,Rob Ainslic akizungumza katika uzinduzi huo usiku huu.
Meneja wa Mipango wa Mradi wa COMMIT,Waziri Nyoni akiwafafanulia jambo waandishi wa habari (hawapo pichani)kabla ya uzinduzi wa Filamu ya CHUMO inayoelezea athari za ugonjwa wa Malaria nchini,Katika hoteli ya Movenpick jijini Dar usiku huu.
Stelingi wa Fimumu hiyo,Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari namna alivyoweza kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya ugonjwa Malaria.
Mkuu wa Masoko na Ushirikiano wa Benki ya Stanbic,Abdallah Singano akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ushirika wao katika Mpango wa kudhibiti malaria kwenye ujauzito wakati wa uzinduzi wa filamu mpya inayoelezea athari za ugonjwa huo katika jamii.
Mtengenezaji Maarufu wa Filamu za Kiafrika zikiwemo NERIA na YELLOW CARD,John Riber (kulia) akiwa na Dada Jackie Karanja.
Wadau.
Wageni waalikwa toka sehemu mbali mbali walihudhulia uzinduzi huo uliofanyika usiku huu katika hoteli ya Movenpick jijini Dar.

Waweza tembelea mtandao wa Filamu hiyo kwa Link hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad