Rahel Manoti, mmoja kati ya waalimu wa shule ya sekondari ya Mkonjowano, pamoja baadhi ya walimu wengine, wakitazama kwa furaha, sehemu ya vitabu vya msaada vilivyotolewa na Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa shule nne za mkoa huo. Ikiwa ni katika kutimiza juhudi za kusaidia jamii hapa nchini, Airtel imekabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za sekondari Mkonjowano, Naputa, Mkundi na Nachunyu, ambazo kila moja imepokea vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja. Makabidhiano ya msaada huu yalifanyika wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara jana.
Haidari Athumani, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mkonjowano, akiwasomea wanafunzi wenzake kurasa ya moja ya vitabu vya msaada vilivyotolewa na Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa shule nne za mkoa huo. Ikiwa ni katika kutimiza juhudi za kusaidia jamii hapa nchini, Airtel imekabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za sekondari Mkonjowano, Naputa, Mkundi na Nachunyu, ambazo kila moja imepokea vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja. Makabidhiano ya msaada huu yalifanyika wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara jana.
No comments:
Post a Comment