Timu ya Mashabiki wa Arsenal wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Bia ya Castre Lager,Kabula Nshimo (tatu shoto,waliosimama) mara baada ya kunyakua Ubingwa wa Castre Beach Football Bonanza,uliofanyika jana katika ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.

Timu ya Mashabiki wa Arsenal wakishangilia ubingwa wao walioupata kwa ushindi wa matuta katika Bonanza la Castre Football lililomalizika jana jioni katika fukwe ya Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.

Nahodha wa Timu ya Mashabiki wa Arsenal akipokea Kombe kutoka kwa Meneja wa Bia ya Castre Lager,Kabula Nshimo mara baada ya kutawazwa ubingwa huo wa Castre Beach Football Bonanza.

Mwali akikisubiriwa kukabidhiwa kwa mabingwa huku akiwa amenakshiwa na vitu vya Shampein.

Washindi wa pili katika Castre Beach Football Bonanza,walikuwa ni Mashabiki wa Liverpool (Bwawa la Maini) ambao walikabidhiwa vilaji vya Castre lager pamoja na mpira ambao utatumika katika michezo mbali mbali watakayokuwa wakicheza.

Mashabiki wa Chelsea walishika nafasi ya tatu.

Timu ya Mashabiki wa Man City ilijinyakulia nafasi ya nne.

Huku nafashi ya Tano ikichukuliwa na Mashabiki wa Timu ya Man Utd ambao walichapwa vibaya sana na kila timu,sijui ni furaha ya ubingwa walioupata huko EPL?

Kamati ya Michezo ikiweka sawa matokeo ya michezo yote.

DJ Manywele akifanya mambo yake huku akipigwa tafu na Mdau.

Burudani ya Sarakasi ilichukua nafasi yake.

Kikosi cha Mashabiki wa Bwawa la Maini.

anapigwa chenga matata mpaka anajikuta akiruka samasoti.

Patashika nguo kuchanika hapa.

Mtanange wa Mashabiki wa Man City na Mashabiki wa Chelsea.

Hapa hupiti hata kwa dawa.

Kituuuuuuuuuu........ hii ndio raha ya Bwawa la Maini,yaani kwa kufunga magoli mazuri tuu hatujambo.

Mie na Mdau Trisher ambaye ni mnazi mkubwa sana wa ile timu iliyoshika nafashi ya pili katika ligi ya EPL.

Wadau wa TBL wakiwa katika picha ya Pamoja.

"eehhh... vipi huko?? haa..!! tushafungwa ngapi??" Kayanda na Washkaji.

Mie kati nikiwa na Wadau wa TBL,Kulia ni Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli na kushoto ni Meneja wa Redd's Premium,Victoria Kimaro

Mnazi wa Chelsea akiwa na kibendera chake kichwani.

Taswira za hapa na pale hazikukosekana.

Wadau wa TBL.

Meneja wa Bia ya Castre Lager,Kabula Nshimo (kati) akiwa na maswahiba zake.

Watu kibao walifurika katika fukwe ya Mbalamwezi.


Mipango ikiendelea.



No comments:
Post a Comment