
nipo mkoani Tanga kwa shughuli mbili tatu, na nilifika sehemu flani na nikajikuta nikivutiwa na madafu yaliyokuwa yamesheni katika moja ya miti ya minazi,nikaomba walau nipate moja lakini wenyeji wakaniambia kuwa kama unaweza kupanda,basi chukua hata yoote.hapo ndipo kidume nilipotaka kuonyesha umahiri wangu na kulekea mtini.hivyo mpaka nalipata hili shughuli niliipata ya kutosha.

si mnaona ninakoelekea??

hapa leo ni mpaka kieleweke,maana siwezi kupoteza hamu yangu kirahisi rahisi.

kukwea mnazi ni kazi kweli kweli.........si mnaona wenyewe jamani??
Mkuu ni kazi sana kwa sisi ambao hatujazoea, lakini kwa wenyewe walio kolea na kazi hiyo, ni kama kumsukuma mlevi tu...anaanguka ki ulainiiiii....!!!!!
ReplyDeleteNiliona Zanzibar jamaa wakikwea nilibaki mdomo wazi, jamaa ni kazi yao ya kila siku.
lakini hatujakuona kileleni ukilizungusha dafu au umeishia kati???!! sema kweli mtaa kwa mtaa!!! manake kama unapanda mnazi ukiangalia chini huendelei!! mdau Leicester uk
ReplyDelete