
Salam,
Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote waishio Reading UK walioweza Kuja Vincent kuchangia wahanga wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa muda wa saa moja tumekusanya Jumla ya pesa taslim Pounds £200 Pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali. Tafadhali Kumbuka bado hujachelewa kwa wakazi wa Reading ambao hawakuweza kufika leo mnaweza kupeleka michango yenu Vincent siku ya mwisho ya kukusanya ni jumanne ijayo tarehe 1.3.11.
Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, MRS NASIBU NA Utawala wa Vincent Restaurant Reading kwa kusaidia zoezi la leo.
Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni







No comments:
Post a Comment