HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 30, 2010

Matakata Sinza "A" Hatimaye yameondolewa

Ndugu Othman,

 Tunashukuru kwa kuweka kwenye mtandao wako ile jumatatu Kero ya jinsi uchafu ulivyokuwa umeachwa majumbani kwetu Sinza kwa zaidi ya mwezi na wiki kadhaa. Hatimae, nadhani wahusika walisikia kilio chetu kwa kupitia mtandao huu. Jana matakataka yamezolewa na saa hizi tunafurahi kuwa tunaingia mwaka mpya na harufu safi. 

Tunaomba adhabu ya kuachiwa matakata isirudie tena kwa mwaka huu mpya wa 2011. Tunamshukuru Mungu kero hii imetoka na tunaomba isirudie tena. Nadhani kuna uongozi wa juu uliliona hili na wahusika wakalifanyia kazi. Katika maoni kulikuwa na malumbano makubwa ,lakini yote yalilenga katika kujenga na sio kubomoa.

Wanasinza Hoyeee!!! Mungu atabariki sote tuanze mwaka mpya 2011 kwa furaha na Shange na Mafanikio mengi. Harufu Mbaya MWIKO!

Mdau wa Sinza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad