HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2010

Wadau Mbali Mbali wa Makampuni Washiriki Kupima Ukimwi Leo

Bosi mkuu wa TBL,Robin Goetzsche akichekiwa damu na mtaalam kutoka Maria Stopers,aliefahamika kwa jina la Peace Kayoza wakati wa kuadhimisha siku ya Wakuu wa Makampuni kupima afya zao na kuwahamasisha wafanyakazi wao kucheki afya zao,iliyofanyika leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Charted,Jeremy Awori akichukuliwa damu tayari kwa kupimwa afya yake wakati wa siku ya Wakuu wa Makampuni kucheki afya zao iliyoadhimishwa leo katika nchi tano za Afrika Mashariki wakati nchini imefanyika katika viwanja vya Karimjee.
Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi nae alishiriki katika mchakato huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB,Dr. Charles Kimei pia alishiriki katika zoezi hilo la kucheki afya katika siku ya Wakuu wa Makampuni kucheki afya zao na kuhamasisha wengine kucheki afya zao.
Nae Mkuu wa libeneke la nanihii katika kitengo cha Nanihii pia alishiriki katika zoezi hilo la kucheki afya na kukutwa yuko gado kama kawa.
Rajab Mhamila a.k.a Super D akifanyiwa mambo katika mchakato wa kucheki afya leo katika viwanja vya Karimjee.
Wadau wa Benki Standard Charted,Anna Makanza (shoto) na Juanita Mramba wakiwakilisha katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi (shoto) akiwa katika mazungumzo Mkurugenzi wa kupambana na Ukimwi katika Shirika la Kazi Dunia (ILO),Sophia Kisting (kati) pamoja na Mdau mwingine mara baada ya kongamano la kuwahamasisha Wakuu wa Makampuni kucheki afya zao,iliyofanyika leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Wadau wa FEMA pia walikuwepo kuwahamasisha watu mbali mbali kuweza kucheki afya zao.
wadau mbali mbali wakisubiri zamu yao ifike ili waweze ingia kucheki afya zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad