HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2010

tanzania next model kufanyika novemba 27

Baadhi ya washiriki wa Tanzania Next Model wakiwa katika picha ya pamoja pindi walipokutana katika kiota cha Mzalendo Pub.Picha kwa hisani ya Jane John.


MWANAMITINDO bora atakayekuwa Tanzania Next Top Model anatarajiwa kulamba kiasi cha sh milioni moja sambamba na kupelekwa chuo cha mitindo.

Mkurugenzi wa Smilling Faces, Caroline Zayumba, alieleza kuwa licha ya mshindi huyo kujipatia kitita hicho cha pesa atapelekwa katika Chuo cha Informative Modelling Management kilichopo Nairobi kusomea masuala ya Mitindo.

Hivyo amewataka wanamtindo wanaoshiriki katika shindano hilo lililoanza katika ukumbi wa Millennium Tower kuchangamkia nafasi hiyo kwa ajili ya kuboresha kipaji chao.

Zaidi wa wanamitindo 14 tayari wamekwishajitokeza katika shindano hilo la mitindo la aina yake hapa nchini ambapo fainali yake inatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu eneo la Funkys Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad