
Kiongozi wa msafara wa madaktari 13 kutoka nchini India, Radhey Mohan akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dares Salaam Jana Jioni.

Baadhi ya madaktari kutoka hospitali za Apollo nchini India wajadiliana mambo mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dar es Salaam jana jioni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Blandina Nyoni (wa pili kushoto) na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa wa kwanza kushoto wakizungumza na baadhi ya madaktari kutoka hospitali za Apollo nchini India, (aliyevaa tisheti ya bluu ni aliyenyoosha mikono) ni Dk. Somasepchar Reddy daktari ambaye ni daktari bingwa wa mifupa na viungo,. Ujumbe wa madaktari hao watakuwepo nchini kwa muda wa siku saba kwa ajili ya kutoa matibabu ya magonjwa ya saratani, moyo, figo, mishipa ya fahamu na mifupa na viungo kuanzia kesho Jumanne.
No comments:
Post a Comment