HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 7, 2010

TIGO WAKABIDHI BASI LA SHULE KWA SHULE YA MSINGI SINZA


Kwa niaba ya Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi,Bw.Benjamin Kulwa akikata utepe kuashiria kukabidhiwa rasmi kwa gari (basi) lililotolewa na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo kwa uongozi wa shule ya msingi ya Sinza Maalum mchana wa leo,kulia akishuhudia ni Afisa Lasimilimali watu wa Tigo,Bwa. Bannet Kakorozya .
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakilipanda basi hilo kwa furaka kabisa

Afisa Lasimilimali watu wa Tigo,Bwa. Bannet Kakorozya akimkabidhi ufunguo wa gari Mkuu wa shule ya msingi Sinza Maalum leo mchana,Bwa.Charles Kataga,gari hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani 71,250 ambazo zinakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni mio moja na sita.Tigo imejitolea kununua gari hilo jipya litakalotumika kwa shughuli za kusafirisha wanafunzi wa shule ya serikali ya Sinza Maalum iliyopo chini ya Manispaa na Wizara ya Elimu pia TAMISEMI.

Kushoto ni basi la zamani ambalo ni chakavu kabisa lililokuwa likitumiwa na wanafunzi wa shule hiyo hapo awali kabla ya kukabidhiwa basi jipya kulia pichani na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo leo mchana.

Afisa habari wa kampuni ya Tigo Jakson Mmbando akizungumza na mama Mariam ambaye ni mmoja wa walezi wa shule hiyo na pia mratibu wa hafla fupi ya kukabidhiwa kwa basi shule hiyo iliofanyika leo mchana na kuhudhuriwa na baadhi ya wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo na wengineo.

Baadhi ya Maofisa wa Tigo wakiongozwa na baadhi ya walimu wa shule hiyo,wakiwa kwenye moja ya darasa la wanafunzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza,wakijionea shughuli mbalimbali zifanywa na wanafunzi wa shule hiyo leo mchana,wakati wa hafla fupi ya kukabidhi basi la shule kwa uongozi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad