HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 29, 2010

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi aagwa leo

Bw. Eliseta Kwayu akiiaga Bodi ya Baraza hilo pamoja na wafanyakazi na katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam kulia ni mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Emmanuel Kija Kamba na kushoto ni mama Freita Kwayu.
Katibu Mtendaji Mpya wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Anaclet Kushuliza akizungumza na wajumbe wa baraza hilo pamoja na wafanyakazi wakati wa kumuaga katibu mtendaji aliyestaafu Bw Eliseta Kwayu aliyekaa (kushoto) katikati ni mke wa Mzee Eliseta Kwayu mama Freita Kwayu.
Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Emmanuel Kija Kamba akisalimia na Mama Freita Kwayu Mke wa Katibu Mtendaji wa zamani wa taasisi hiyo Bw Eliseta Kwayu katikati aliyestaafu utumishi wa uma katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam kushoto ni Katibu mtendaji mpya wa baraza hilo Bw Anaclet Kashuliza.
Wafanykazi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakimkabidhi zawadi katibu mtendaji mpya wa baraza hilo Anaclet Kashuliza wakati wa hafla ya kumuaga katibu Mtendaji aliyestaafu utumishi wa umma Eliseta Kwayu.
Wafanyakazi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakiserebuka
Afisa Mwandamizi wa Uwekezaji katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Edward Kessy kushoto akisalimiana na mkurugenzi wa Uaezeshaji wa baraza hilo Bi Joyce Chonjo katika Hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mtendaji aliyestaafu Bw. Eliseta Kwayu iliyofanyika kwenye Hoteli ya City Paradise jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad