HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 15, 2010

jengo la kwanza lililojendwa kwa gharama kubwa duniani

Mukesh Ambani, ni tajiri bilionea kuliko wote nchini India, na pia ni tajiri wa nne kwa thamani katika levo za dunia. Ambani amejijengea jumba la kuishi lenye thamani za Dola Bilioni za Kimarekani.


Jumba hili lina ghorofa 27 ambazo ukizizungukia zote kwa siku moja basi unamaliza mahitaji yako karibu yote bila kutoka nje ya mjengo huo. Mukesh amesema kwamba hili ni jumba la kuishi yeye, mkewe kipenzi, na watoto wao watatu (Hapa lazima mwafrika apige kelele).

Katika jumba hili kuna sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi na kutunza afya kwa ujumla, mahala pa kuchezea dansi penye ukubwa kama wa klabu zetu tunazozifahamu hapa nyumbani, madimbwi kadhaa ya kuogelea (swimming pool), ukumbi wa kutazamia senema unaoweza kubeba watu 50 kwa wakati mmoja, vyumba kibao vya wageni (mwafrika sijui ataendelea kulalama kwenye hili?), na mwisho kabisa ni varanda zenye ukubwa wa kucheza sarakasi kabisa.

Ukitaka kufika nyumbani kwa bwana Mukesh, unaweza kutumia usafiri wa aina mbalimbali. Kama unajua wazi kwamba foleni za India zitakufanya uwe unasonya njia nzima basi unaweza kuchukua helikopta, pale nyumbani kwa bwana Mukesh kuna viwanja vitatu kwa ajili ya usafiri huo. Kama namna gani vipi umenunua gari mpya na unataka kwenda nayo kumlingishia bwana Mukesh usitie shaka, ana uwanja wa kuegesha magari 160 kwa wakati mmoja.

Ukishuka kwenye gari au kipepeo (helikopta) chako kuna lifti tisa zinakusubiri wewe uende kokote katika ghorofa hizi 27, kwa hiyo dada zangu msitie shaka, komeleeni michuchumio ile ile ya mwaka.

Cheki mpango mzima wa huu mjengo katika picha hapo chini.


Kutoka FotoBaraza.Me

--
Bob Sankofa
fotobaraza.me

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad