Habari mkuu, nina swali moja ambalo naomba uweke ktk globu ili wadau waweze kulizungumzia, Hivi kwanini nchini Tanzania kuna viwango vikubwa sana vya mawasiliano ya simu ya ndani ya nchi tofauti na nchi nyingi duniani. Mfano kama ukiweka credit ya Tsh 10,000/= basi utakuta hiyo pesa inakwisha ktk muda mchache sana.
Pili kuna viwango vikubwa sana vya kupiga simu kati ya mtandao mmoja kwenda ktk mtandao mwingine, mfano TIGO kwenda Zain, n.k. Hivi viwango ni vikubwa sana tena sana na ambavyo havina maelezo yakinifu na ya ndani yenye kuleta maana ya hizo gharama! Ukiweka 10,000/= na kupiga kwenda ktk mtandao mwingine basi credit zako zitakwisha kama mazingaombwe!!! Ndani ya dakika chache!!!
Katika swala lingine la kuchekesha, TIGO wameanza ku-charge watu wenye mtandao sawa (TIGO kwa TIGO) wenye kutaka kutuma salio (credit) kwenda kwa ndugu na marafiki wenye simu za TIGO (TIGO kwa TIGO).
Mwanzo ili swala lilikuwa bure, cha kushangaza tar 07th October 2010 jioni walitoa notice ya muda mchache yenye kusema kwamba kuanzia tar 08th October 2010 TIGO wataanza kucharge 3% ya kuwango chochote cha pesa unachotuma kwenda kwenye simu nyingine ya mtandao wa TIGO.
Huu ni wizi wa wazi wazi kwa wananchi wa Tanzania ambao ni masikini!! Hiyo 3% ukizidisha mara milioni 3 au zaidi ya wateja wa TIGO si fahida ya bure kwa kampuni ya TIGO!!!? Ili swala lingetakiwa liwe bure kama good gesture kwa wateja walio chagua mtandao wa TIGO!! Ningeomba wahusika waliangalie hili swala.
Wakati umefika kwa Serikali kuingilia kati swala hili la mawasiliano, Serikali ifanye kazi kama walivyo ingilia swala la bei ya Mafuta nchini Tanzania kupitia EWURA.
Tungeomba Serikali, TCRA, Providers wote wa simu, wadau wote waweze kuliangalia ili swala kiundani, tunahitaji maendeleo lakini sio kumnyonya Mtanzania ambae ni masikini. Viwango vya bei zenu za simu hazikubaliki KABISA!!.
Leo ni swala la simu, next time nitaleta hoja ya bei ya Internet Tanzania.
Nashukuru.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment