
Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini,Nimka Lameck (11) akimkabiz uban kwa mjomba wa mmoja wa watoto waliofarika katika ukumbi wa disco wa Luxery Pub ulioko Wilayani Temeke,jijini Dar.

Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini,Nimka Lameck (11) (katikati) aiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wake pamoja na watoto wa Temeke.
Na Ripota wa Mtaa Kwa Mtaa Blog
Ujumbe maalum wa watoto nchini leo mapema umedhuru kwa ndugu na jamaa waliopatwa na msiba kufuatia hitilafu ya umeme kwenye ukumbi wa Luxery Pub Temeke na kusababisha vifo vya watoto watatu.
Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck (11), Salome Filbert (7),Monica Ntevi.Josephu Nzozi, na Maleo Lameck.
Waliweza kutembea familia ya Mtoto Fatuma Ramadhani (7) ambaye alifariki dunia papo hapo ukumbini humo ambapo mama yake Zaitun Chenja ambapo alionekana kuwa na huzuni huku akisema anamwachia Mungu.
Waliweza kutembelea kati ya familia mbili na kutoa rambirambi kwa wafiwa pamoja na kutoa ujumbe kwa wa wazazi hao kutokata tama, kwani yaliyotokea ni mapenzi ya Mungu.
“Sisi watoto tiliopo hapa na tukiwawakilisha na watoto wenzetu,tunatoa pole sana kwani tumeguswa sana na tatizo hili kwa ujumla na tunaomba sheria kali zichukuliwe dhidi ya wahusika” walisema watoto hao.
Aidha, ujumbe huo pia ulitembelea kutoa rambirambi zao kwa familia ya Lilian Rajabu (9) ambaye naye alizikwa juzi na walitoa pole kwa ndugu na jamaa sambamba na kutoa ubuni wao.
Hata hivyo pia ujumbe huo uliweza kutembelea ukumbi wa Luxery Pub na kujionea jinsi palivyo, ambapo walitoa sera yao na kukemea vikali kwa tukio hilo. Baadhi ya watoto ambao walishuhudia tukio hilo.
waliweza kutoa maoni yao na kuomba Serikali kuimalisha ulinzi siku za sikukuu kuweka ulinzi mkali ikiwemo kwenye baa na kumbi za starehe ilikupunguza matatizo kama haya yanayotokea kwa watoto.
“Tunakumbuka mwaka 2008, tukio kama ili lilitokea na kuweza kuuwa watoto 19, mkoani Tabora, hivyo hatutaki tena kushuhudi vifo vya watoto wenzetu vikiendelea kutokea kwani hawana hatia” walisema baadhi ya watoto waliokuwa na umri miaka 15/17 ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili na tatu wakazi wa Temeke.
Mpaka sasa Serikali imeunda tume maalum kuchunguza Sakata hilo huku mmiliki wake akiwa anashikiliwa na jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment