HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 22, 2010

tigo wazindua kituo cha huduma kwa wateja temeke

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo, Temeke eneo la Mtoni kwa Aziz Ali jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando na wanne kushoto ni Meneja Matawi ya Tigo,Innocent Mayawa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Chiku Gallawa (kushoto) akijisajili na huduma ya Tigo Pesa muda mfupi baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Temeke, Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa kituo hicho, Josephine Reuben wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando na katikati ni Meneja Matawi wa Tigo, Innocent Mayawa.
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Tigo, David Kagusa (kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa mara baada ya mkuu huyo kuzindua kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Temeke, Dar es Salaam jana.

1 comment:

  1. siku hizi bongo baada viongozi kufungua sehemu za kutoa huduma kwa jamii kama vile vituo vya matibabu au mabomba ya maji, imekua pilikapilika za kufungua biashara ambazo hazisaidii wananchi wenye kuhitaji huduma za jamii.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad