HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 15, 2010

Ridhiwani Kikwete aendeleza libeneke kusini

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akivishwa skafu na chipukizi Asha Khalifa alipowasili Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM, Kata ya Njinjo, Hemed Kipembekile alipowasili Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapiduzi Tanzania Bara na Visiwani, Profesa wa Siasa Mtopa Ali Mtopa akitoa nasaha zake katika mkutano wa ndani wa viongozi wa UVCCM, Wilaya Kilwa, uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete (katikati), mjini Kilwa Masoko,juzi. Ridhiwani na makada wengine wa UVCCM wameanza ziara ya kuhamasisisha vijana kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkubwa. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM,Mkoa wa Lindi Hassan Masala.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akihutubia katika mkutano Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad