BENDI ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music Band, inatarajia kufanya onyesho la aina yake katika Ukumbi wa TCC Chang'ombe,jijini Dar siku ya Idd mossi mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa Msondo Ngoma, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa onyesho hilo linatarajia kuwa la aina yake.
Amesema kuwa onyesho hilo linatarajiwa kuanza mapema ili kuweza kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa muziki huo.
Amesema kuwa katika onesho hilo pia Msondo Ngoma itaimba nyimbo mbili mpya ambazo hazijawahi kusikika mahali popote.
Amesema kuwa nyimbo hizo ambazo wamezitunga wakiwa kambini Amana Ilala wakati walipokuwa katika mfungo wa Ramadhan.
Aliendelea kumesema pia bendi hiyo itaimba nyimbo mbalimbali za zamani pamoja na zile mpya ambazo zitakuwepo katika albam yao inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.
"Tunatarajia kufanya onesho la aina yake wakati wa siku kuu ya Idd kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wetu baada ya kupumzika kwa mwezi mzima wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan" alisema Super D.
Msondo Ngoma Baba Ya Muziki, siku ya Iddy Pili wanatarajia kufanya onyesho jingine la aina yake katika Ukumbi wa Gymkhana Klabu uliopo Zanzibar.

No comments:
Post a Comment