
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi kinyago Miss Tanzania 2010 Geneviev Emmanuel kama sehemu ya kwenda kuitangaza nchi yetu,Mlimbwende huyo anatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China ambako mashindano hayo yatafanyika.

Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi Miss Tanzania 2010 Geneviev Emmanuel kifuko kilichokuwa na CD ya mambo ya Utalii na vitu vingine ikiwa kama sehemu ya kwenda kuitangaza nchi yetu.

Meza kuu,toka kulia ni Mkuu wa Sekta Binafsi nchini,Ester Mkwizu akifuatia Vodacom Miss Tanzania,Genevive Emmanuel, Mkurugenzi wa Utamaduni na Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Prof. Helmas Mwansoko namwisho ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania,George Rwehumbiza.

Vodacom Miss Tanzania 2010,Genevive Emmanuel akielekea sehemu yake ya kukaa mara baada ya kutoka kujisevia msosi katika hafla fupi ya kumuaga na kumkabidhi bendera ya Taifa ili akaiwakilishe vyema nchi katika mashindano ya urembo ya Dunia yatakayofanyika Beijing,China hivi karibuni.

Vodacom Miss Tanzania 2010,Genevive Emmanuel akiwa na mgeni rasmi katika hafla hiyo,Ester Mkwizu wakati wa kuchukua chakula mchana wa leo.

Mkuu wa Itifaki Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akipiga stori mbili tatu na Mtaalam wa Mambo ya Habari wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakati wa hafla ya kumuaga mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 anaetarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China kwenye mashindano ya Dunia.

baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo leo.
No comments:
Post a Comment