
"ndugu yangu hapa mambo yanazidi kuwa magumu tufanyeje?" hivi ndivyo wanavyoonekana askari hawa wa kikosi cha zimamoto cha First mara baada ya kujitahidi kadri wanavyoweza ili kuweza kuuzima moto uliokuwa unawaka kutokana na mabaki ya kipira ya kutengenezea kandambili a.k.a malapa yaliyokuwa yamerundikwa katika kiwanja ya mpira yakitokea katika kiwanda cha kutengenezea kandambili hizo cha OK Plasti LTD kilichopo huko Vingunguti leo.moto huo inasemekana kwamba ulianza kuwaka kidogo kidogo na baadae kupamba kama uonekanavyo pichani hapo,inasadikika kwamba kuna mtu atakuwa aliuwasha lakini hajulikani ni nani.

Kikosi cha zimamoto cha kampuni ya First kikiwa katika harakati ya kuuzima moto huo uliokuwa upamba kwa kasi ya ajabu kutokana na upepo mkali uliokuwepo eneo hilo.

moto umepamba kweli kweli.......

Gari za zimamoti zikibadilishana nyingine ikitoka kwenda kufata maji kwa ajili ya kuuzima moto huo ambao kama wasingefanikiwa kuuzima moto huo basi hasara kubwa ingetokea katika kiwanda hicho na vile vya jirani kwani moto huo ulikuwa ni mkali sana.

Watoto wakijisevia mabaki hayooo

mabaki ya kandambili yakiwa yamerundikwa katika kiwanja cha mpira huko Vingunguti.
No comments:
Post a Comment