
Akizungumza na Jiachie jijini Dar jioni hii kiongozi wa kundi hilo Rich One amesema kuwa baada kuikamilisha albamu yao yenye jumla ya nyimbo kumi,kwa sasa wanajipanga vyema kuitambulisha albamu hiyo itakayojulikana kwa jana la POA TUA, vile vile utakwenda sambamba na uzinduzi wa Logo na tovuti itakayokuwa na habari zao mbalimbali zikiwemo na kazi zao kama vile vyimbo na video zao.
"Tumeamua kuja na mambo mapya baada ya kimya kidoogo kwa wapenzi wetu,kama nilivyosema hapo awali albamu ina jumla ya nyimbo kumi,ambazo baadhi yake ni Poa Tu, Mapenzi Matamu, Apple, Moyo Wangu, Zaga Zaga na nyingine nyingi," alisema Rich One na kuongeza kuwa albamu hiyo imesheheni mahadhi tofauti tofauti kama vile Zouk, R&B pamoja na Hip Hop.
Rich One amesema kuwa ndani ya albamu hiyo amewashirikisha wasanii kadhaa mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipa,kama vile Chidi Benz,Kitokororo wa FM Academia,Hard Mad,Chiku Keto,Mh Themba na wengineo.
Kundi hilo linaloundwa na wakali akiwemo Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p).
No comments:
Post a Comment