HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 9, 2010

Twiga Stars vs Seattle Sounders


Picha ya pamoja wachezaji wa Twiga Stars na Seattle Sounders

Twiga Stars usiku wa kuamkia leo wamecheza na timu ya Seattle Sounders ya wanawake katika mchezo wa kusisimua ambapo wageni walifungwa bao 4-2 katika uwanja wa Starfire Sports Complex jijini Tukwila, WA, nchini Marekani, mbele ya mashabiki wa Seattle Sounders fans na Watanzania wanaoishi maeneo hayo.

Sounders ndio walioanza kupata bao dakika ya sita na kupata la pili dakika chache baadaye. Dakika 40 ya mchezo Twiga walikuwa wameshafungwa bao 3-o, lakini wakarejesha moja kabla ya mapumziko kupitia kwa winga wake machachari Mwanahamisi Omary kwa kona iliyoenda wavuni moja kwa moja.

Kipindi cha pili Sounders walianza kwa nguvu na kupata bao la nne baada ya kipa wa Twiga Stars kutema mkwaju mkali ambao mfungaji aliuatia na kufunga. Asha 'Mwalala' Rashidi alifunga bao la pili kwa kichwa baada ya kona safi ya Eto Mlenzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad