
wanafunzi wa shule ya msingi Lutihinda iliyopo Kigogo wakiwa wamezunguka vibanda vya wauza pipi na biskuti vilivyopo nje ya shule hiyo.katika lundo lote hilo waweza kuta ni mmoja tu ndio mnunuzi wa kinachotakiwa kununuliwa hapo na wengine woote wakawa ni waombaji tu.hivyo ndivyo inavyokuwa katika kipindi hiki cha shule ya msingi na wengi wetu tumepitia haya.

hawa nao wakiwa wamebeba dawati lao toka kwa fundi aliopo jirani na shule hiyo mara baada ya kuleta mushkeri,sasa sijui ni nani aligharamia swala zima la ufundi wa dawati kule kwa fundi??maana kwa kwendo huu ni kama waliamua wenyewe kulipeleka kwa fundi baada ya kuona wanataabika na ilihali linaweza kufanyiwa marekebisho.
No comments:
Post a Comment