
"Utotoni nilifunzwa kurejesha mambo kwa kasi ile ile yafanyikapo kwa pande zote. Yaani kwa uharaka nilionao wa KUKOSOA basi niwe nao KUSIFIA na kama niwezavyo KULALAMA niweze KUSHUKURU pia.
Najua ndugu wewe ungenikosea ningekueleza na ndio maana NAKUSHUKURU kwa kutofanya hivyo.
Ni kweli kuwa leo Aug 10 ni mwaka mpya wa maisha yangu. Wengine huita Birthday. Na katika kuishi kwangu nimejifunza mengi toka kwa watu wengi na kwa namna nyingi. Na si kila anifunzaye huniweka katika nafasi ya kuweka kumbukumbu kwani si kila nijifunzalo ni la hiari ama kwanjia njema.
Lakini kwa wale wanifunzayo kwa wema, nami kuona nia njema ya kuendelea kujifunza, basi kila niwezapo huwa naweka kumbukumbu.
Ina maana mimi kuwa na anwani yako ni kielelezo tosha kuwa nimepata kutembelea kazizo na kwa kukutembela huko nilijifunza na ama ninajifunza na ama nitaendelea kujifunza.
Napenda kukushukuru kwa kile ulichoongeza katika mchakato wa maisha yangu na nakuombea mafanikio ili uelimishaji nilioupata kwako uwaguse wengi na kuifaa jamii.
ASANTE KWA KUWA WEWE.
Blessings
No comments:
Post a Comment