HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 16, 2010

clouds entertainment yatoa msaada kituo cha mama theresa

Mully B akipewa mkono wa shukurani kutoka kwa mmoja wa wanaoelelewa na kituo hicho.
Kampuni ya Clouds Entertainment Ltd leo mchana imetoa msaada wa vyakula mbalimbali vikiwemo mchele,mafuta ya kupikia,unga na vinginevyo katika kituo cha kulelea watoto wenye matatizo mbalimbali wakiwemo watu wazima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati,jijini Dar.Clouds Entertainment iliwakilishwa na Mtangazaji wa Clouds FM Lumuliko Mengele a.k.a Mully B (aliyebeba mtoto) pamoja na Said Bonge (shoto pichani) a.k.a Bonge Barabarani.Muwakilishi wa zoezi hilo la utoaji misaada amesema kuwa lilikuwa rasmi wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 lililoisha hivi karibu.Mully B alisema kuwa mikoa kadhaa kampuni ya Clouds Entertainment Ltd kupitia tamasha la Fiesta tayari imekwisha toaa misaada kama hiyo kwenye vituo vya watoto yatima, ikiwemo Dodoma,Tanga,Mwanza na kwingineko ambako tamasha hilo lilikwisha fanyika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad