
Meneja wa bia ya Kilimanjaro (TBL) George Kavishe akifafanua jambo mbele ya wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010 katika nyanja mbalimbali,kwenye semina elekezi ya lala salama iliofanyika leo jioni kwenye hotel ya Paradise,jijini Dar

Muwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Mzee Angelo Luhala akifafanua kuhusu kwa baadhi ya wanamuziki ambao wameamua kujitoa kwenye tuzo hizo kwa sababu wanazozijua wao,aidha ameongeza kwa kuwashauri wanamuziki kuwaheshimu mashabiki na wapenzi wao waliowachagua,"hawapaswi kuwaangusha kwa namna moja nyingine,kikubwa ni kuonesha na kukubali thamani yao kwako,Wanamuziki tusikubali kujiangusha wenyewe kwa mambo ambayo wakati mwingine yanakuwa hayana maana"" alisema Mzee Luhala.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Plus Commonication ambayo pia ni moja ya waratibu wa tuzo za Kili Music Awards 2010,Fina Mango akifafanua jambo na pia kumkaribisha muwakilishi kutoka baraza la sanaa la Taifa,kufafanua baadhi ya mambo kwenye semina ya wasanii waliochaguliwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hizo,ambazo safari hii zimekuwa na muonekano mpya na wenye msisimko mkubwa kwa wanamuziki wenyewe na hata wapenzi/washabiki wa muziki hapa nchini.
No comments:
Post a Comment