HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 9, 2010

Miaka Miwili ya FotoBaraza.Net Kuadhimishwa Kesho Chadibwa Beach Resort

Mpendwa mdau, kama unavyoona katika countdown yetu ndo hivyo tena, tumebakiza masaa tu kabla hatujaanza kusherehekea mwaka wa pili tangu kuzaliwa kijiji cha FotoBaraza.

Kesho, Jumamosi, wanakijiji waliotoa michango yao ya TSHs. 20,000/- tutajumuika pale Chadibwa Beach Resort, Kigamboni, ili kula, kunywa, kuogelea, kufanya michezo mbalimbali, kukata keki ya mwaka wa pili wa Kijiji, kuonana ana kwa ana na wanakijiji wengine, kucheza muziki, na kujadiliana nini kimepungua na nini kinahitaji kupunguzwa.

Iwapo ulichelewa kutuma mchango wako usihofu, njoo na buku 20 (TSHs. 20,000/-) yako kwenye eneo la tukio na tutakula bata mpaka kuche.

Milango itakuwa wazi kuanzia mapema saa nne ya asubuhi. Nini cha kuvaa ni juu yako mwenyewe hata ukiamua kuja umevaa nepi ni poa tu.

Kwa wale watakaokuja na magari ni vyema kufika feri mapema maana siku za wikiendi huwa kuna msongamano mkubwa sana wa magari, kila mtu anataka kwenda kula bata Kigamboni. Kwa watakaochapa lapa (watakaokuja kwa mguu) msijali sana, kuna vivuko viwili vinapiga kazi masaa 24 pale.

Heri ya Mwaka Mpya wa kijiji cha FotoBaraza. Tukutane pale.

Pamojah!

Nenda FotoBaraza katika

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad