HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 12, 2010

King Kif Tena Katika Nyanja Ya Utamaduni

Kimasa kutoka www.kingkif.blogspot.com huku kifua changu kikiwa mbele nachukua mtaa ndani ya www.othmanmichuzi.blogspot.com nikiwa na masuala ya utamaduni na jinsi yanavyoweza kusababisha maendeleo kwa jamii yetu ya Tanzania.

Kwa ufafanuzi wangu utamaduni ni jumla ya mambo yote yanayobuniwa na jamii husika ili kukidhi utashi na maendeleo yake ama ni mwenendo wa maisha ya kila siku ya jamii.

Hapa kuna mtazamo wao wa mambo, taratibu zao za kuendesha maisha ambazo zinawatofautisha wao na jamii nyingine.Utamaduni wa jamii husika ndio kitambulisho kikuu cha taifa lolote na ni kielelezo cha utashi na uhai wa watu wake.

Hivyo basi, tafsiri hii inaonyesha kuwa jinsi utamaduni unavyohusika na mchakato mzima wa maisha ya mwanadanu sambamba na maendeleo yake kiuchumi.

Basi bwana, ili kuhakikisha kazi za sanaa na utamaduni unatoa mchango muhimu na kuleta maendeleo serikali yetu inapaswa kuweka sheria na kanuni mazubuti katika maeneo ya ughramiaji , hadhi na kutoa fursa zamafunzo kwa wanautamaduni .

Hili likifanyika vema wanautamaduni watapiga hatua kutoka walipo na kufika juu zaidi katika sanaa , mikakati , mipango na itakuwa ni dira sambamba na kupunguza umasikini.

Serikali inaweza kuondoa kodi katika vifaa vya kitamaduni na iache kuviona kuwa ni vya anasa na isimamie sheria ya hakishiriki na hatimiliki , pia inaweza kushirikiana na wasanii , mafundi katika uzalishaji kuwekeza katika utamaduni ama kudhamini.

Aidha, serikali inao uwezo wa kuwapatia wanautamaduni wataalamu kutoka nje ya nchi ili kutoa mafunzo ya teknolojia mpya kuhusu bidhaa ,masoko na jinsi ya kufanya utafiti kwenye tasnia hii.

Isitoshe wazalishaji na wasanii nao ni vema wakatambua kuwa wao ni washiriki wakuu kwenye eneo hili na wanaweza kupata kipato kikubwa kuliko sasa na kuwa wanachangia uchumi wa taifa .Inabidi pia waongeze kuheshimu kazi zao katika kuzifanya kikamilifu , waoneze ubunifu
katika kila kazi zao mpya na wahakikishe kazi zao mpya zinauzika.

Tanzania Bara baada tu ya kufanikiwa kupata uhuru mwaka 1961, serikali ya Mwalimu Nyerere iliainisha matatizo makuu matatu ya wakati huo kuwa ni umasikini , ujinga na maradhi.

Tangu litoke tamko hilo serikali hile ilielekeza nguvu kwa namna mbalimbali katika kupambana na matatizo hayo makuu matatu, huku ikitoa msisitizo kwa kubadilika badilika kadri muda ulivyokuwa unasogea.

Ni vema sasa serikali ya awamu ya nne ikaipa aula tasnia ya utamaduni ili kuwatoa wasanii wetu hapa walipo.

Ni mimi Kimasa kutoka
www.kingkif.blogspot.com

unaweza kucheki nami
kwa kupitia simu : 0714-077040
ama
email kingkif07@gmail .com.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad