Ni kweli kwamba sisi Watanzania wote ni wadau wakubwa wa lugha ya
Kiswahili. Ni kweli pia kwamba wote kwa pamoja tumekuwa tukifurahi na
kucheka kila tunaposikia kwamba lugha hii inaelekea kuwa lugha ya
kimataifa.
Pia, naona ni vema hapa mwanzo nikamuunga mkono Rais wa kwanza wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mwalimu Kambalage Nyerere kwa
kuifanya lugha hii kuwa lugha ya taifa ambapo imeweza kuwa lugha ya
kufundishia katika shule za msingi.
Mpango wake huo ni mzuri na ni wakizalendo.Mpango huo umesaidia kwa
namna pana kuifanya lugha hii kuwa adhimu hapa duniani.
Lakini , kwa sasa Watanzania tunapojivunia kukuwa na kusambaa kwa
lugha ya Kiswahili nnje ya Tanzania ambapo ina maanisha kukuwa na
kusambaa kwa mila na destuli zetu kwa wakati huu, tunajukumu kubwa
kuhakikisha kiswahili kinabeba maneno na misamiati mingi ya lugha zetu
za Kibantu ili iwe kielelezo cha kweli kwa utamaduni wetu.
Hii itakuwa ni muhimu kwetu Watanzania na Wabantu wote kwa ujumla.Huu
mpango wa wakati huu wa lugha yetu ya Kiswahili kuwa na maneno ambayo
ni nusu ya Kiarabu na robo nyingine ni Kireno, halafu robo nyingine
sijui ya Kizungu gani ? Tutakuwa tunajivunia lugha ya Kiswahili huku
nyuso zetu zikiwa na aibu kwa wenye maneno na misamiati yao yaaani
Warabu na wazungu!
Hebu tazama maneno kama oganaizeisheni , ishirini , thelasini ,
arobaini, meza na mengine yapo mengi tu ambayo tumeyatohoa kutoka
kwenye lugha ya kiaarabu na kizungu.
Hivi kweli hatuna maneno kama haya kwenye lugha zetu za Kibantu? Mbona
kuna makumi mawawili , makumi matatu , makumi manne n.k.
Hebu tuweke na tutumia maneno haya ya Kibantu ili sisi Waswahili wa
Tanzania tuongoze kwa Kiswahili fasaha na sanifu ambapo nadhani hata
Wabantu wengine wote wataanza kujivunia.
Ni mimi Kimasa kutoka mtandao wa www.kingkif.blogspot.com ama kwa
mawasiliano zaidi utanipata kwa 0714-077040 email
-kingkif07@gmail.com.

Hongera King kif kwa hoja yako ya kizalendo, ila kwa miaka hii kila Mtanzania anataka kuongea kwa kuchanganya maneno ya Kiingereza na Kiswahili kwa wakati mmoja! Mfano siku moja jaribu kusikiliza kikao chochote cha Bunge, utaona kilicho mtoa nyoka pangoni mwake!
ReplyDelete