UONGOZI WA TASABA CHINI YA RAIS FIDELIS MSOMEKELA KWA MASIKITIKO MAKUBWA UNATANGAZA MSIBA WA KAKA YETU IMRAN MTUI ULIOTOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 31 JANUARI.
UONGOZI WA TASABA UKISHIRIKIANA NA MJUMBE WA UBALOZI WA TANZANIA INDIA WANAFUATILIA TARATIBU ZOTE ZA MSIBA.
KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA VIONGOZI WA TASABA NAMBA ZAO A SIMU ZIPO KWENYE KICHWA CHA UKURASA HUU (BOFYA HAPA).
MHESHIMIWA RAIS FIDELIS AMEWAOMBA WATANZANIA KUWA WATULIVU MUDA HUU WA MSIBA NA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KUHAKIKISHA TUNAMALIZA MSIBA HUU SALAMA.MSIBA HUPO KWA DADA HAKIKA
ADDRESS
3RD FLOOR
1ST MAIN
GOPALA REDDY LAYOUT
BANASWADI
BANGALORE-78
INDIA
3RD FLOOR
1ST MAIN
GOPALA REDDY LAYOUT
BANASWADI
BANGALORE-78
INDIA
MUNGU AILAZE ROHOYA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.
----------------------------------------
Mwanafunzi Mtanzania,
Imran Mtui auawa India
Habari zilizopo katika blogu ya Watanzania waishio Bangalore (TASABA), pia katika mtandao wa Twitter zinathibitisha kuwa, mwanafunzi wa Kitanzania, Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo kishiriki Cha Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa hauna kichwa.

Taarifa zinasema kuwa mwili huo ulikutwa kando kando ya reli katika eneo la Shivajinagar katika mji wa Bangalore ukiwa hauna kichwa huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya. Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
"Mimi nilipata taarifa hizo juzi jioni ambapo jana tulifanya kikao na wenzangu na kumtuma Ofisa wetu Mzee Amon Mwamanenge na mwanasheria wetu wamekwenda huko kupata undani wa tukio hilo," alisema Balozi Kijazi.
Alisema kuwa kwa sasa hawezi kutoa picha kamili lakini mwili wa kijana huyo umekutwa ukiwa hauna kichwa na mguu umebondeka. Kijana huyo aliyefariki alikuwa amemaliza Shahada ya Usimamizi wa Biashara (BBM) na alitambulika kwa jina la Imran Mtui. Aliwahi kuwa Mtunza Fedha wa Chama Cha Wanafunzi wa Kitanzania Waishio Bangalore (TASABA).
Habari hizi zimedhibitishwa na mdogo wa marehemu, Issa Mtui, kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Marangu, Moshi. Alieleza kuwa mwili wa marehemu unategemewa kuwasili nchini Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya taratibu za mazishi ambayo yatafanyikia Marangu.

Imrani ni wa pili kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia hiyo. Inadaiwa kuwa kabla mauti haijamkuta alitarajiwa jana angekuwa amerejea nchini baada ya kuwa amechukua vyeti vyake vya masomo ambavyo alikuwa akivisubiri baada ya kuhitimu masomo yake.
Polisi nchini India wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
Polisi nchini India wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
------------------------------------------------
Kwa niaba ya wadau wote, Blogu yetu ya Mtaa Kwa Mtaa inatoa pole kwa wafiwa na kuwaombea wawe na subira wakati huu mgumu. Mola ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi
- AMINA
- AMINA

Inaniuma sana kifo cha kaka yangu mpendwa ndo alikuwa tegemezi kwnye familia yetu ameniacha katika majonzi makubwa sana mungu ailaze roho ya marehemu pema pepon
ReplyDeleteGlory Mtui
mmm jamani india mafia wapo wengi isije ikiwa aliletea foul na wenzake kibiasha au kikazi, maana tunajua india watu wengi wanatumia shule kama cover up tu lakini kuna mambo yanayoendelea
ReplyDelete