HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 24, 2010

Serengeti Breweries Yazindua Kampeni Ya "Funga Goli"

Meneja Mkuu wa Uhusiano, Habari na Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda akiongea na waandishi wa habari leo.

***********************************************

Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua kampeni katika kanda ya ziwa, lengo likiwa ni kuhamasisha mshikamano wa watanzania kwa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’ kuelekea mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Uhusiano, Habari na Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda, amebainisha kuwa raha ya mchezo wa soka ni kufunga magoli ama ushindi. Hivyo akawataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi ili kuiwezesha timu ya taifa kufunga magoli katika mechi hiyo.

Kampuni ya bia ya Serengeti, ambao ndio wadhamini wakubwa wa ‘Taifa Stars’ mpaka ifikapo mwaka 2011 wakati huu wataendesha kampeni hiyo maalumu ijulikanayo kama ‘Funga Goli’ katika mkoa wa mwanza.

Mapunda ametoa wito kwa wakazi wa Mwanza kutembelea katika baa za karibu ili kushiriki katika kampeni hiyo na kupata fursa ya kuwa miongoni mwa washindi watakaojinyakulia zawadi mbalimbali. Miongoni mwa zawadi hizo ni fulana, kofia, bia pamoja na kujishindia tiketi ya kushuhudia mechi baina ya Taifa Stars na The Cranes katika uwanja wa Kirumba hapo tarehe 3 Machi 2010.

Siku wa mchezo huo wa soka, kutakuwa na maandamano ya barabarani (Road Show) katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza na yataishia katika uwanja wa soka wa Kirumba.

Kampeni hii inazinduliwa kwa mara ya kwanza kanda ya ziwa katika jitihada ya kuiunga mkono Taifa Stars. Kampuni ya bia ya Serengeti inawatakia kila la kheri watanzania wote kuishangilia na kuiunga mkono time yetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad