HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 15, 2010

Miss Tanzania,Miriam Gerald Azidi Kusota Sero


Kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Hashim Lundenga ‘Anko’ leo imekwaa kisiki kumtoa ‘selo’ mrembo anayeshikilia taji hilo kwa msimu wa mwaka 2009/10 Miriam Gerard, ambaye anasota katika gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam tangu Ijumaa iliyopita akikabiliwa na mashitaka ya ushambulia na kuharibu mali.

Lundenga, wapambe wake pamoja na ndugu wa Miss huyo, walionekana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, mapema leo wakihaha kutaka kumuwekea dhamana, lakini taarifa za kuaminika zinadai kuwa hekaheka hizo ziligonga mwamba baada ya kutokuwepo kwa askari magereza ambaye angewasilisha hati ya dhamana ambayo ingewezesha mrembo huyo kuachiwa kutoka katika gereza hilo.

Uwezekano mkubwa uliopo ni Miriam kuendelea kusota selo hadi kesho atakapofikishwa mahakamani hapo kwa mara nyingine kwa ajili ya kushughulikia dhamana yake.

Miriam anashikiliwa pamoja na mpenzi wake Kenedy Victor ‘Kenny’ kwa tuhuma za kumfanyia vurugu Bwana Mushi pamoja na kuharibu vyombo vyake vya muziki vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi laki saba.

Walipofikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, walikosa dhamana hali iliyosababisha watupwe mahabusu hadi Februari 25 mwaka huu.
Habari na picha kwa hisani ya GPL

1 comment:

  1. Hiyo hapo haijakaa vizuri watapelekwaje mahakamani bila askari magereza? Kweli Bongo Tambarale............

    ReplyDelete

Post Bottom Ad