HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 28, 2010

Flava Nite @ Mzalendo Pub,Palikuwa Hapatoshi

Mdau Chidy akimzawadia Wine mwanadada alieizungusha nyonga kiukweli ukweli(mwenye top nyeusi hapo kati) huku marafiki zake wakimshangilia kwa ustadi wake huo.huyu dada hii ni mara ya pili anaramba mzigo huo.
Bob Chidy naona alinogewa maana ngoma imemalizika lakini yeye bado anataka mambo yaendelee,sijui ingekuwa vipi kama zingeongezwa kama dakika nne hivi? mambo ya kunyongesha yamekolea.
usisubiri kuhadithiwa mambo haya,hebu ibuka j,mosi moja pale Mzalendo Pub ujionee kwa macho yako mambo haya,maana ni uhondo mtupu walahi. Ringi limekolea,yaani hapo ni full kuduarika tuu. kitu cha kwaito hicho toka pande za kwa mzee Madiba,hapo ni mwendo wa kwenda kwa step tuu na ukizubaa umetolewa nje ya ulingo.
magoma yamepamba moto,hakuna anaetaka kukaa tena hapo.

Kila Jumamosi ndani ya Mzalendo Pub kuna Dicso la ukweli kupitiliza,ambalo liko chini ya maDJ wakali na makini sana hapa Bongo.ambao si wengine bali ni Dj Bon Love,Dj Mackay pamoja na Dj Oscar.Mdau kama ulikosa J,Mossi hii basi fanya hima usikose j,Mossi ijayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad