HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 18, 2010

Ulishawahi Lisikia Neno Swagga???

Niaje wewe Dogo Mzurukaji,naomba niwekee hii hapo kwako ili wadau waweze changia kidogo mada hii.maana mimi imekuwa ikinitatiza kwa muda sasa.

Neno SWAGGA limekuwa maarufu sana hapa kwetu nchini na duniani kote, kama ni mfuatiliaji sana wa Masuala ya burudani na Ma Superstar ni dhahiri utakuwa umeshawah kulisiki hilo neno. Ki ukweli sina uhakika asili ya hili neno lilipotokea au kuanzishwa ila limetokea huko ughaibuni kwa wenzetu, kwani nilishalisikia katika nyimbo nyingi za wasanii wa Kimataifa NA Watu maarufu katika nyanja za burudani wakiongozwa na wamerekani zaidi.

Hili neno SWAGGA limeenea na kufika hapa kwetu nchini na linatumika mpaka kwa watu wasioelewa maana yake halisi, sio kwamba nasema halina maana nzuri laaah hasha..! naomba mnielewe vizuri waungwana. Baada ya maelezo hayo marefu naomba kuuliza swali...

Hivi mbona kulikuwa na neno kama hili kabla ya kuja hilo La kizungu na lenye maana sawia na matamshi sawia na hilo
Kwa wale watu wa zamani nawa sasa hivi walio makini watakuwa wanalifahamu..

Mfano: Tuliswaga rumba , tuliswaga mguu, na mifano mingine kama hiyo unayo iweke tafadhali tukumbuke.

JE HIVI HATUTHAMINI VYA KWETU MPAKA TULETEWE NA WAZUNGU? KWANI HIVI SASA KILA MTU UTAMSIKIA MY SWAGGA IZ ON...

NI HAYO TU.
SWAGING LIKE THIS YO....

Ni mimi wako mswahili mfurukutwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad