HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 7, 2010

OMBI LA KUPUNGUZA SIKUKUU NCHINI TOKA KWA MDAU

Ndugu umewahi kukaa na kujiuliza Mtanzania wa kawaida anayefanyakazi
Serikalini na baadhi ya sekta binafsi ana pumzika siku ngapi kwa
mwaka ? Umewahi kuhesabu kuna sikukuu ngapi zinazotambuliwa na
serikali ambazo zinalazimisha mfanyakazi huyu akapumzike nyumbani ?

Ukiacha sikukuu hizo Mfanyakazi huyu anakuwa na likizo ya karibu mwezi
moja kila mwaka kama mkataba wake wa kazi unavyosema hapo jumlisha na
siku zake za kuumwa , siku za kwenda Kwenye misiba ya ndugu jamaa na
marafiki na siku zingine za sherehe za kiofisi ?

Ukijumlisha sikukuu zote hizo pamoja na siku zingine za likizo misiba
ETC unaweza kupata Mtanzania wa kawaida anakaa karibu mwezi mmoja
unusu kwa mwaka bila kufanya kazi , jumlisha na masaa aliyotegea kwa
kulala makazini au kuchelewa kufika huko makazini unaweza ukashangaa
sana .

Kwa hali hii naomba kutoa ombi la kupunguzwa sikukuu na siku zingine
za mapumziko kwa Nchi yetu pamoja na kurekebisha sheria zingine wa
kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi.

Mdau Mzalendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad