HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 28, 2010

Kibaka Achezea Vitasa Vya Maana Leo Mtaa Wa Lumumba

wananchi wenye hasira kali kama za Nyati wakimtembezea vitasa(kipigo) kibaka aliesadikiwa kuiba mzigo wa jamaa.hii imetokea mchana wa leo katika mtaa wa Lumumba pembeni mwa jengo la ushirika.
"hebu nipisheni nimuonyeshe huyo kibaka,tutahasira nao sana hawa"
"hatulali wana kutembea kwa amani hapa mjini kwa ajili yenu,kula hii"
yaani ilikuwa kupiga na kumpisha mwingine ili nae ajinome kumsulubu kibaka huyo,aliemshika kibaka huyo ndie mwenye mali iliyotaka kuyoyoma.mbona palikuwa hapatoshi leo pale Lumumba.
"hebu ntengee huo uso nikupe za Cheka fasta fasta"hivyo ndiovyo alivyokuwa akisema jamaa huyu
pembeni pale ndio mzigo uliotaka kuingia mitini na kibaka huyu.
wananchi waliofika katika eneo la tukio wakimdekshia kibaka huyo ambae baada ya kichapo cha maana alipata upenyo na kula kona kwa spidi ya mnyama duma.Daah jamaa naona ule upenyo ulimpatia hafueni sana maana kile kichapo kilikuwa si cha mchezo.hii imetokea mchana huu katika mtaa wa Lumumba ubavuni mwa jengo la Ushirika na benki ya Access.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad