HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 18, 2010

Hoja Ya Haja

Ndugu wadau,
Binafsi nimeshitushwa sana na taarifa ya vifo vya watu 14 plus 17 kujeruhiwa na hali zao ni mbaya kutokana na kuvamiwa na majambazi huko kisiwani Ukerewe. Naogopa kuiita Tanzania ni nchi ya amani.

Hivi hapo amani ipo wapi? Kuna tofauti gani na Sudan? Kuna tofauti gani na Somalia? Au kuna tofauti gani na yale yaliyotokea Kenya? I am very sorry to say this, but sina kumbukumbu nzuri kama nchi ina waziri wa mambo ya ndani? Kama yupo, yumkini ni marehemu.

Hili suala la majambazi linasumbua kila mahali nchini. Lakini taarifa anayopelekewa Rais asome kwenye hotuba ya mwisho wa mwaka ni eti ujambazi umepungua kwa kiasi kikubwa, na pongezi kwa jeshi la polisi.

Kwa hali ilivyo nchini,tunafika mahali tunaishi kwa woga mkubwa pasipo kujua ni nani wa kutulinda kwakuwa serikali yenye jukumu la kulinda maisha ya watu wake bado haijapata njia sahihi ya kuwalinda watu wake.

Je itakuwa ni jambo jema kama kila mtu atanunua bunduki yake? Ili ikitokea yanakukuta tu unasimama kidete kivyako! Au kila mtanzania apate mafunzo ya kijeshi ili inapotokea unakuwa na mbinu zote za kulikabili. Manake ukipiga simu polisi, watakwambia gari halina mafuta au watakuja masaa mawili baada ya majambazi kuondoka.

Ndugu zangu, ni njia gani nzuri ya kujiweka salama na familia zetu? Manake usalam tunaodhani upo kimsingi haupo. Amani tunayoihubiri, kiuhalisia haipo.

tulijadili kwa kina hili ndugu zangu

Mdau Kafyulilo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad