
Kocha wa timu ya Yanga a.k.a vijana wa mtaa wa Jangwani na Twiga street,Kostad Clinton akiwa amebebwa juu juu na mashabiki wa timu ya Yanga mara baada ya kumalizika kwa gemu baina ya watani zao wa jadi Simba S.C katika uwanja wa Taifa.

Kikosi cha Yanga kilichoitembezea kichapo cha 2-1 timu ya Simba jioni hii katika uwanja wa Taifa a.k.a shambani kwa Babu

hizi tu zinatosha kusherehekea nazo Xmas watani zetu.

baada ya kumalizika kwa mpira tu na bendera ikatupwa mtaroni na dogo huyu akaiokota na kuitangaza ili kama yupo alieitupa aje kuchukua bendera yake.

mashabiki wa Yanga wakikatiza mtaa wa Congo kuelekea ilipo klabu ya Simba pale mtaa wa Msimbazi.

Yanga! Yanga! Yanga!...............

yaani mbona rahaaaaaaaa.......
Timu ya Yanga a.k.a Watoto wa Jangwani imetoa zawadi nono ya Xmass kwa wapenzi wake kwa kumbanjua mtani wake wa jadi Simba kwa bao 2-1 kwenye nusu fainali za kombe la Tusker Cup.Alikuwa ni Jerry Tegete aliyeweka chuma cha kwanza mnamo dakika ya 72 na baadae kijana machachari Shamte Ally aliweka kimiani bao la pili nyavuni kwa wapinzani wao wa Jadi Simba zikiwa zimebaki dakika tatu kabla ya muda wa dakika 120 kumalizika.kwa ushindi huo Yanga itamenyana na Sofapaka kutoka nchini Kenya katika fainali ya mashindano hayo ya Tasker siku ya jumapili tarehe 27/12/2009.haha ahah ahaha ahaha.... Yanga Bwana
No comments:
Post a Comment