
nguzo ya simu ambayo waya wake ulikuwa umekatiza katikati ya matawi mti ikiwa imeangukia gari na kupasua kioo,mara baada ya jamaa walioamua kuyapunguza matawi ya mti huyo kukata tawa ambalo liliwa ni kubwa na kuifanya kuzo hiyo ambayo ilikuwa imeoza kupita kiasi kushindwa kuhimili uzito wa tawi hilo na kuanguka.

msela akiteremka toka juu ya mti mara baada ya kusababisha madhara kutokana na kazi aliokuwa akiifanya ya kukata matawi ya mti ambayo yalikuwa ni marefu sana kiasi kwamba hata nyaya za simu na umeme zilikuwa chini ya matawi hayo.

kwaambaali upande wa kulia ni muhusika wa gari hilo akisikitika kwa lilitokea kwa wakati huo huku akiiangalia gari yake kwa uzuni mkubwa.

Askari wa usalama barabarani akiandika maelezo ya tukio hilo lililotokea siku ya jana katika mtaa wa Sunna ndani ya Magomeni mapipa.
No comments:
Post a Comment