
"Nikiwa katika mandhari tulivu yenye upepo mwanana wa Ufukwe wa bahari ya Hindi kisiwani Unguja.Unguja ni Njema Atakaye na Aje, Raaaaha Mustaarehee..Burudaaani Kabisa nani anasema Unguja kuna purukushani, purukushani za Unguja huanzishwa na watu wa Bara wenyewe ni wakarimu na watulivu, hula pamoja, huingia misikitini pamoja na hata mazungumzo yao ni mamoja, tena ukichunguza zaidi takribani wote ni wanandugu, huyu kaoa mtoto wa yule na yule kaoa mtoto wa huyu, Binamu kamuoa binamu mwenzie...ugomvi wa huku unachochewa na wengine si waunguja asilani!!!!"hayo si maneno yangu bali ya huyu Mwanafasihi Rashid Mkwinda ambaye ndiye mwendesha kijiji cha Fasihi Za Ufasaha kinacopatikana kwa kubonyeza
HAPA hebu mtembelee hapo mtaani kwake uone mambo yake.
No comments:
Post a Comment