
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na warembo kutoka mataifa mbalimbali wakati alipowakaribisha Ikulu jana kwa chakula cha jioni, warembo walipata nafasi ya kumuuliza rais maswali mbalimbali kuhusu mambo mbalimbali ya jamii uchumi michezo na mengine mengi.

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na warembo watakashiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka Miss East Africa na kamati nzima ya mashindano hayo mara baada ya chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu jana, warembo hao kutoka mataifa saba wanatarajia kupanda jukwaani kesho tarehe 18/12/200 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, mshindi wa shindano hilo atajinyakulia gari aina ya Toyota Celica Sports yenye thamani ya dolla 24,000.
No comments:
Post a Comment