HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 8, 2009

Msondo Kuzindua Albamu Yao Mpya Leo

Waimbaji wa bendi ya Msondo music band wakiimba wakati wa onesho lao lililofanyika Dar es salaam jumamosi iliyopita siku ya Media Day,Msasani Beach Club.kushoto ni Eddo Sanga na Isihaka Kitima 'DJ Papaupanga'
Wanamuziki wa bendi ya msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa michezo mbalimbali ilioyowakutanisha waandishi wa habari jana kushoto ni Roman Mn'gande Romario na Hamisi Mnyupe.(Picha na Rajabu Mhamila)


Na Mwandishi wetu

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bandi Leo watafanya utambulisho wa albam yao mpya ya Huna Shukrani kwa staili ambayo haijawai kufanyika nchini

Msemaji wa bendi hiyo ndg Rajabu Mhamila 'Super D' ameliambia gazeti tando hili kwamba uzinduzi huo utafanyika leo jumanne Desemba 8, katika ukumbi wao wa Nyumbani uliopo Amana,Ilala

Alisema katika uzinduzi huo bendi ya African Star wana wa 'Twanga Pepeta' yenye mashabiki lukuki ndani na nje ya nchini watawasindikiza ndugu zao wana Msondo Ngoma katika uzinduzi wao huo.

Akielezea maandalizi zaidi Mhamila alisema licha ya kusindikizwa na bendi hiyo pia wamejipanga kutoa zawadi kwa mashabiki wao, ambapo kila mpenzi atakaekata tiketi ya kuingia ukumbini atapewa zawadi ya albam yao mpya,

Alisema nyimbo zitakazotambulishwa siku hiyo ni pamoja na wimbo uliobeba albam hiyo, Huna Shukrani uliotungwa na Saidi Mabera,Kiapo (husein jumbe), Haki Yangu Iko Wapi (Uluka Uvuluge), Mama Cos, uliotungwa na Marehemu (Joseph Maina), Albino (Juma Katundu),Machimbo Isihaka Kitima (dj papa upanga) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)

Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad