Kwanza kabisa tunapaswa kumshukuru Mungu muumba wa mbingu na ardhi pamoja na vyote vilivyomo ndani yake kwa kutujaalia afya njema katika kipindi kizima cha mwaka 2009 na tuzidi kumuomba kwa kila hali ili aweze kutujaalia zaidi na zaidi katika kipindi kijacho cha mwaka 2010 na kuendelea,kwani yeye ndiye muweza wa yoote.
Wadau wangu watukufu wa Blog ya Mtaa Kwa Mtaa,napenda kuchukua fulsa hii kwa siku ya leo kutoa salamu zangu za dhati kwenu ikiwa ni katika kipindi cha msimu wa sikukuu ya Krismas na huku tukijiandaa kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2010 ambao siku chache tu zijazo tutakuwa tumeshaufikia.
Hivyo basi kama kuna tuliyokoseana katika kipindi kilichopita basi yapaswa tusameheane kwani hayo yaweza kuwa ni mapungufu ya kibinadamu kwan i kusameheana kwetu ndio muendelezo mzuri wa maisha yetu na kwa yale mema tuliyoyafanya kwa kipindi hicho basi tusiyaache na tuyaendeleze zaidi na zaidi.
Wadau wapendwa naomba kuwaasa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kuwa watulivu kabisa katika kusherehekea kwetu kwani ni mambo mengi huwa yanatokea katika kipindi hiki,hivyo basi yatupasa kujipanga vizuri na tusherehekee kwa amani na utulivu sherehe zetu hizi,kwa ya mungu ni mengi na laweza tokea lolote la kutokea.
kwa haya machache naomba niwatakie sikukuu njema ya Krismas na makaribisho mema ya mwaka mpya wa 2010 wadau wangu woote na popote mlipo katika Dunia hii,bila kusahau naomba niwape nafasi nanyi wadau kuweza kutuma salamu zenu za sikukuu kwa yeyote umpendaye,naomba mtume salamu zenu kupitia email hii
nami nitazifikisha kwa walengwa kama kawa.nasema tuko PamoJah.
-Othman Michuzi
-Othman Michuzi
No comments:
Post a Comment