HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 4, 2009

Ajali Maeneo Ya Kimara Buncha Asubuhi Hii

gari aina ya Suzuki Vitara (sikufanikiwa kushika namba zake za usajiri) likiwa limepinduka ndani ya mtaro mkubwa uliopo pembezoni mwa barabara ya Morogoro Road,katika eneo la Kimara bucha.gari hii ilijikuta ikiingia mtaroni humo mara baada ya gari aila ya Coaster (daladala) kulazimisha kuingia upande wa pili wa barabara bila ya ishara yoyoye na kusababisa dereva wa gari hii aina ya vitara kutaka kujaribu kumkwepa na kujikuta katika hali hii.daladala lenyewe ni hilo hapo ambalo liko chini ya usimamizi wa Askari Polisi ambao kwa bahati nzuri walikuwepo jirani kabisa na eneo lilipotokea tukio hilo.
wakazi wa eneo hilo la Kimara Bucha wakiiangalia gari iliyoingia ndani ya mtaro baada kupigwa pande na daladala lilipokuwa likihama njia bila ya ishara yeyoye asubuhii hii.
hakuna mtu alieumia katika ajali hii iliyotokea asubuhi hii katika barabara kubwa ya Morogoro Road.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad