HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 17, 2009

Miss Utalii Kinondoni 2009 Yazidi Kupamba Moto

Washiriki wa Miss Utalii Kinondoni 2009 wakiwa katika mapozi ya picha mwishoni mwa wiki iliyopita katika fukwe ya coco beach
Warembo wakiwa katika Pozi la pichi
Wamenyooka na wanafaa kuwa mabalozi wa utalii wa ndani,lakini mmoja wao ndiye atakayeibuka na taji la Miss utalii kinondoni 2009.


MWAKA WA NEEMA, WADHAMINI WAZIDI KUMIMINIKA MISS UTALII KINONDONI

Kampuni ya Ele-Tech & Equipment kwa kushirikiana na kampuni ya Tan Country Power Systems ltd za jijini Dar es Salaam, zimejitokeza kuungana na Baadhi ya Makampuni katika kusaidia shindano la Miss Utalii Kinondoni kwa kusaidia masuala mbali mbali yakiwemo mavazi na zawadi kwa Washiriki katika siku ya Fainal.

Aidha kampuni hiyo itagharamia gharama zote za jukwaa litakalotumiwa na warembo siku hiyo,hivyo kufanya jumla ya udhamini wao kuwa wa thamani ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000).Hatu hiyo imekuja siku ,moja tangu kampuni ya Mashujaa Pub & Entertainment na AL WATER WELL DRILLERS kwa kushirikiana na Kampuni Kubwa kabisa ya Usafirishaji ya Mamaa Sakina Trans zote za Vingunguti kujitokeza pia kudhamini shindano hilo kwa kiasi cha shilingi milioni mbili.

Zaidi ya warembo 17 wamejitokeza katika Mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2009/2010 –Kinondoni,ambao wanaendelea na kambi ya mazoezi katika ukumbi wa New Msasani Club Kinondoni Dar Es Salaam chini ya mwalimu wao Ester Kinyunyu ambaye ni Miss Utalii Tanzania 2005/2006 -Iringa.

Kuanzia mwishoni mwa wiki hii warembo hao wataanza ziara maalum za kutembelea ,kujifunza na kutangaza maeneo mbalimbali ya kitalii,kitamaduni na kihistoria yaliyopo katika wilaya ya Kinondoni,baada ya jumapili iliyo pita kutembelea kivutio cha ufukwe wa Coco Beach uliopo Oysterbay jijini.

Maeneo watakayotembelea ni pamoja na Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama,soko la sanaa za mikono la Mwenge na eneo la biashara la kimataifa la Mlimani City la jijini.Shindano la Miss Utalii Tanzania 2009/2010 – Kinondoni ni mfululizo wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2009/2010 yanayofanyika katika ngazi mbalimbali za Wilaya,Mikoa na Kanda zote nchini,ambapo washindi wa wilaya hushiriki katika fainali za mikoa,washindi wa mikoa hushiriki katika fainali za kanda na washindi wa kanda watashiriki fainali za Taifa za 2009/2010,huku washindi wa Taifa wakiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya Miss Tourism World 2009/2010,Miss Heritage World 2009/2010 na Miss United Nations 2009/2010.

Shindano la Miss Utalii Tanzania 2009/2010 –Kinondoni litafanyika siku ya Ijumaa tarehe 27-11-2009 katika ukumbi wa ndani wa kisasa na wa kitalii wa New Msasani Club uliopo karibu na Ubalozi wa Marekani Drive Inn Cinema,Maandalizi yanakwenda vizuri, na litakuwa ni onyesho la karne la nyota tano ambalo litahudhuriwa na viongozi na watu mbalimbali wa mashirika ya umma,binafsi na serikali kitaifa,kimkoa na kiwilaya.

Mkurugenzi wa Ele-Tech & Lihting Agency , Kibo Merinyo, ametaja baadhi ya sababu za kudhamini shindano hili kuwa ni pamoja na kuvutiwa na mfumo mzima wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania,ikiwemo wa kuwafundisha washiriki kucheza na kuimba nyimbo na ngoma za asili za makabila mbalimbali ya Tanzania jambo ambalo ni adimu katika mashindano mengine kuonekana.

Wadhamini wengine ni pamoja na Empire Ferniture, Clouds Fm, A-one Tours & Safari, Aurora Security, The Grand Villa Hotel, Mashujaa Pub, Mamaa Sakina Trans, Mlonge By Makai Enterprisess, Daja Saloon, Fitness Centre, Vam General Supply, Mh Idd Azan, New Msasani Klabu, Chicken Hut Tanzanian ltd, Chagga Bite, Savannah Lounge, Kampala International Univarsity(KIU),Michuzi Blogs & Kitangoma Magazine, Angels Galapo , na Raimbow Social Klabu.

Warembo waliojitokeza na ambao wapo kambini hadi sasa ni Joseline Sekwao,aike Abel,Neema Mashalla,Jackline Mollel,Ratifa Bakari,Christina Masandeko,Zubeda hamisi,Robby Masandeko,Agness Selis,Juliana Johnson,Sauda Ramadhan,Barke Mohamed,Faraja Hassan,Matha Denis,Sarah Shaaban,Lulu Dello,Sophya Dei.

Asante,
Shaaban Mpalule
Mkurugenzi Miss Utalii Tanzania,
Wilaya ya Kinondoni

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad