HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 19, 2009

Huruma Jamani


huyu Mama yuko pale selander brige pembeni ya kituo cha polisi cha hapo selander,kiukweli Mama huyu anasikitisha sana hasa kutokana na ile hali yake ya kufuata gari na kuomba msaada kwa alie ndani ya gari hiyo,kinachinifanya nimuonee huruma huyu Mama ni pale taa za barabara hiyo zinaporuhusu magari na yeye anapokuwa anarudi kwenye hilo baraza la katikati,yaani utamuonea huruma kwa jinsi anavyojikokota.jamani kwa nini hawa watu wanaokaa humu mabarabarani wasipatiwe msaada wa kujikwamua kimaisha na waondokane na adha hii ya kukaa sehemu kama hizi ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yao??

2 comments:

  1. Mara nyingu unafanya makosa kuandika -HADDHA badala ya ADHA ambalo ni neno sahihi.
    Mara nyingi habari inakosa umakini unapokosea kuandika katika usahihi wake.
    Naomba ulifanyie kazi hilo, kwani mara zote huwa unakosea hili neno
    Kumbuka tunajifunza kutokana na makosa.
    Wabillah tawfiq

    ReplyDelete
  2. Umefanya vizuri kurekebisha,jua kwamba nafuatilia

    ReplyDelete

Post Bottom Ad