HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 16, 2009

Washkaji Wa Pikipiki Walipomuungia Jamaa Wa Rav 4 Toka Kibamba Mpaka Ubungo

Jamaa wanaoendesha pikipiki za kukodisha maeneo ya Kibamba,jijini Dar walimfukuzia jamaa mwenye gari aina ya Rav4 ambayo ilikuwa haina namba za usajili,baada ya kugongwa kwa mwenzao hukohuko Kibamba ambapo walikwenda nae sambamba mpaka Ubungo mataa na kufanikiwa kumzuia kuondoka hapo mpaka akubali kumlipa mwenzao aliemgonga .kitu ambacho kilisababisha vurugu kubwa sana baina ya mwenye gari huyo na hawa jamaa wa pikipiki.
ilikuwa ni patashika nguo kuchanika siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa,pale Ubungo mataa.maana jamaa wa pikipiki hawakukubali kabisa kuona mwenzao kagongwa hala aliemgonga anaingia mitini huku wakimuona. inaelekea jamaa aliilaani sana taa nyekundu pale Ubungo siku hiyo,maana lilizuka balaa kubwa sana pale Ubungo siku ya Kumbukumbu ya miaka kumi ya kifo cha Baba wa Taifa.mpaka wazee wa feva (Polisi) waliingilia kati swala hilo na kuwataka wakalimalizie sehemu za usalama.
daah hawa jamaa wanamshikamano kweli kweli,hebu cheki mtiti huo wa mapikipiki toka huko Kibamba.picha hizi zote ni kwa hisani ya Mdau Chaoga wa kule Manzese uwanja wa nanihii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad