HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 12, 2009

RODGERS ASHINDWA KWA UTATA!

Na Sunday Shomari
Rodgers Mtagwa aliingia Madison Garden akipeperusha bendera ya Tanzania usiku wa Jumamosi na huku mpinzani wake Juan Lopez akiingia na reggae tong kwa mpambamo wao Rodgers ambaye aliingia akipewa nafasi finyu ya kufanya chochote ameacha gumzo kubwa miongoni mwa washabiki wa ndondi hapa Marekani.

Huku mashabiki wakizomea na wengine kushangilia Rodgers Mtagwa aliuthibitishia Ulimwengu wa Ndondi kwamba yeye si mbabaishaji na hakupewa jina la "Tiger" bure kwani Juan Manuel Lopez alikuwa hajawahi kupigana zaidi ya raundi 10 katika mapambano yake yote yaliyopita isipokuwa hili.

Juan Manuel Lopez aliibuka mshindi katika pambano hilo na kutetea taji lake la WBO kwa pointi 116-111,115-111,114-113 Katika ukumbi wa Wamu Theatre uliojaza watu takriban 3152. Ama kwa hakika Juan Lopez alianza kwa spidi kama kawaida yake na kutoa mashambulizi ambayo kila konde alilorusha alipata majibu yake.

Na kumwangusha Rodgers Mtagwa katika raundi ya pili lakini ambapo Mtagwa aliamka haraka na kuendelea na pambano kitu ambacho yeye Rodgers anasema kuwa haikuwa chochote kwani Lopez alimpiga kwa kumsukuma kwa nyuma ya kichwa na refa pia hakuhesabu huko ni kuangushwa.

Pambano hilo liliisha kwa majaji wote watatu kumpa ushindi Manuel Lopez wakidai alipigana vizuri katika raundi za mwanzo hasa ya kwanza hadi ya sita.

Lakini jinsi mpambano huo ulivyoendelea ndivyo bingwa huyo alivyozidi kuchoka na Mtagwa kuzidi kuongeza kasi ya mashambulizi hasa konde lake la kulia ambalo lilitia dosari kubwa kwenye uso wa Lopez.Katika raundi ya saba Mtagwa alionyesha cheche kwa kuingiza makonde ya kushoto na kulia( Left and right hook) ambayo yaliingia vizuri usoni kwa mpinzani wake na kwa mujibu wa hesabu za computer Compu Box aliongoza raundi hiyo mpaka 8 kwani alikuwa nyuma kwa pointi.

Juan Manue Lopez ilibidi abadilishe staili na kumkalia mbali Mtagwa ambapo alikuwa akiingiza ngumi chache halafu anakaa mbali maana aligundua akikaa karibu anapata matatizo.

Rodgers naye alionywa na kona yake asiruhusu mpinzani wake kukaa mbali bali aendelee kuingia ndani na atumie nafasi ya kujibishana makonde (pound for pound) ambayo ilikuwa ni ngumu kwa mpinzani huyo kufanikisha.

Baadhi ya watu waliokuwa wakimshangilia Lopez tangu mwanzo wa pambano walielekea kubadilisha kibao na kuanza kumshangilia Rodgers kwani katika raundi ya 11 ambapo Lopez alikuwa hoi kabisa akimshika Rodgers ambaye alikuwa akirusha makonde mengi ambayo yaliingia kwenye uso wa mpinzani wake na kumpasua juu ya jicho la kushoto na ilikuwa ni kengele iliyomuokoa Lopez katika raundi ya 11.

Katika raundi ya 12 Mtagwa aliendelea kuwasha moto na huku mpinzani wake Lopez akiendelea kupigana kwa kujihami alimanusura aanguke ila alitumia mbinu na ujanja wa kila aina kumshika Mtagwa na kumkumbatia,kumsukuma na kurusha makonde machache mpaka raundi hiyo ilipokwisha.

Watangazaji waliita staili ya Mtagwa ni "Dirty Fight" wakisema bondia huyu wa Tanzania anapigana staili ya Philadelphia ambako ndiko makazi yake. Baada ya mpambano huo haikuwa wazi nani mshindi lakini baada ya majaji kutangaza baadhi ya watu walizomea kwa kuona Rodgers kaonewa hata yeye mwenyewe alipohojiwa alisema haelewi kwa nini kashindwa pambano hilo .

Naye Lopez kwa upande wake alimsifu Rodgers kuwa ni bondia hatari na lilikuwa ni pambano gumu si kama alivyofikiria na kudai kuwa alichoka kidogo mwishoni mwa pambano hilo.

Watangazaji wa PPV walimsifia Rodgers kwamba ni bondia ambaye ameweza kuonyesha moyo mkuu na hivi sasa watu wengi zaidi watamfahamu na pia anastahili kupewa nafasi nyingine kwani ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa hivyo wanafikiria atapata nafasi ya kuwania taji lingine la dunia au pambano kubwa.

Promota wa Lopez Bob Arum alipulizwa kama atampa nafasi ya marudiano Rodgers alikataa na kudai bondia wake amepata ushindi wa wazi na hahitaji marudiano na Rodgers Mtagwa.Katika pambano jingine la utangulizi la Ubingwa wa WBA (Feather) Yuriokos Gamboa wa Cuba alitetea taji lake kwa TKO katika raundi ya nne dhidi ya Whyber Garcia wa Puerto Rico. Hivi sasa wanaaangalia uwezekano wa kumkutanisha mcuba huyu na Juan Lopez.

Huku Gamboa akidai Lopez hana kitu, Lopez amemwambia akajaribishe moto wa Mtagwa aone kazi yake.

1 comment:

  1. Kashindwa ameshindwa, sio kwa utata. huku Marekani hakuna uswahili. Tusipende moral victories watanzania "wametufunga lakini chenga tumewala".

    Mtagwa anajitahidi and he make me proud as a Tanzanian, Im very sad sababu angepata pesa zaidi angeshinda. Ila hajashindwa kwa utata

    ReplyDelete

Post Bottom Ad